SYRIA-CAIRO

Syria yaridhia mpango wa amani uliopendekezwa na Umoja wa nchi za Kiarabu

Wafuasi wa rais Asad wakiandamana mjini Damascus kumuunga mkono kiongozi wao
Wafuasi wa rais Asad wakiandamana mjini Damascus kumuunga mkono kiongozi wao ®Reuters

Nchi ya Syria imeridhia mpango wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu wa kukoma kwa vitendo vya umwagaji damu uliodumu kwa takriban miezi minane huku bado rais Bashar Al-Assad akiendelea kupata shinikizo la kuondoka madarakani.

Matangazo ya kibiashara

Utawala wa Assad umejikuta katika shinikizo kutoka kwa mataifa ya kiarabu kuunga mkono mpango uliopendekezwa na umoja huo kukomesha machafuko dhidi ya waandamanaji wanaotaka Assad kuondoka madarakani ili kuepuka hali hii kusambaa katika mataifa mengine ya ukanda wa nchi za kiarabu.

Katika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nchi za nje kutoka jumuiya hiyo uliofanyika mjini Cairo nchini Misri, utawala wa syria meridhia kumaliza machafuko dhidi ya waandamanji na kuahidi kufanya mazungumzo na upinzani chini ya wapatanishi toka umoja huo.

Assad ametakiwa kuwaacha huru raia wanaoshikiliwa baada ya kukamatwa kwa makosa ya kuandamana halikadhalika ametakiwa kuondoa vikosi vyake vya kijeshi kutoka kwenye miji mbalimbali nchini Syria ambako kumekuwa na mapigano makali.

Hata hivyo Marekani kupitia msemaji weke Jay Kani, imesema kuwa msimamo wap wa kutaka Assad kuondoka madarakani uko palepale ingawa wanaunga mkono juhudi za kimataifa za kuishawishi nchi hiyi kukomesha mashambulizi dhidi ya raia.