Baraza la kitaifa la nchini Syria laomba ulinzi kutoka kwa jumuia ya kimataifa

Waandamanaji wanaoipinga serikali katika mji wa Homs nchini Syria
Waandamanaji wanaoipinga serikali katika mji wa Homs nchini Syria Reuters

Wapinzani nchini Syria wamehitaji ulinzi wa kimataifa mjini Homs, mji uliozungukwa na vikosi vya rais wa nchi hiyo Bashar Al Assad.

Matangazo ya kibiashara

Wakiuita mji huo kuwa eneo kinara kwa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binaadam, baraza la taifa la Syria limetaka Umoja wa Mataifa, jumuiya ya kiislam na jumuiya ya nchi za kiarabu kuchukua hatua za kukomesha mauaji yanayotekelezwa na utawala wa nchi hiyo.

Taarifa ya upinzani imeitaka jumuia ya kimataifa kupeleka waangalizi wa kimataifa mjini Homs kuangalia kwa ukaribu hali ilivyo nchini humo na kuzuia mauaji zaidi.

Baraza la taifa la nchini humo limetaka pia kuondolewa kwa raia kutoka kwenye maeneo yanayoshambuliwa na yaliyoharibiwa.

kwa siku ya tano mfululizo sasa, utawala wa Assad umezingira mji wa Homs ili kuzuia nia ya wakazi wa mji huo na kuwakabili raia wanaojaribu kupinga amri ya utawala na kusisitiza kupatiwa haki yao ya msingi ya kupatiwa uhuru na utu.