TEHRAN-IRAN

Irani yaishutumu Israel na Marekani kwa vitisho juu ya mashambulizi ya kijeshi dhidi ya mitambo yake ya Nuklia

Mahmoud Ahmadinejad rais wa Iran kwenye kikao cha Umoja wa Mataifa Septemba 22.2011
Mahmoud Ahmadinejad rais wa Iran kwenye kikao cha Umoja wa Mataifa Septemba 22.2011 REUTERS/Eric Thayer

Iran imeishutumu Israel na marekani kitendo cha kuomba kuungwa mkono na jumuia ya kimataifa ili kutekeleza mashambulio ya kijeshi dhidi ya mitambo yake ya Nuklia.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad ameonya hatua hiyo inayotarajwa kuchukuliwa na israeli dhidi ya nchi yake na ameeleza kuwa mpango wake wa Nuklia ni kwa shughuli chanya.

Ahmadinejad amesema kuwa uwezo wa Iran katika kufanikisha mpango wake wa urutubishaji wa Nuklia unakuwa kwa kasi na wenye maendeleo na kwa sababu hiyo imeweza kushindana na ulimwengu na kudai kuwa hivi sasa Israeli na nchi za Magharibi hasa Marekani zinahofu juu ya uwezo wa Iran.

Kauli ya Ahmadinejad imekuja baada ya rais wa Israeli Shimon Perez kusema kuwa uwezekano wa kuishambulia Iran kijeshi upo karibu kuliko uwezekano wa kidiplomasia.
Rais huyo wa Israeli anashikilia kigezo kuhusu ripoti ya shirika la kimataifa la Nyuklia inayo tarajiwa kutolewa siku za usoni kuhusu nguvu za nyuklia za Iran.

Ufaransa tayari imeitahadharisha Israeli kuhusu mashambulizi yoyote dhidi ya Iran.