Syria

Umoja wa Mataifa waonya kuhusu hali inayoendelea nchini Syria

(REUTERS)

Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu hali ya machafuko inayoendelea nchini Syria kama ile iliotokea nchini Libya. Hii ni baada ya idadi kubwa ya wanajeshi wa Syria waliotumwa kuwasambaratisha waandamanaji kukiuka amri hiyo na badala yake kujiunga na wananchi.

Matangazo ya kibiashara

Navy Pillay mkuu wa kitengo cha haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa ameonya kwamba hali inayo jiri kwa sasa nchini Syria ni ya kutisha, na kwamba kilichotokea nchini Libya kinaweza pia kutokea nchini Syria.

Pillay ameyasema hayo kwenye baraza la uslama la Umoja wsa Mataifa wakati akiwasilisha ripoti kuhusu ulinzi wa raia katika maeneo yanayo kumbwa na mizozo.

Hayo yanatokea wakati serikali ya Syria imeendesha mashambuliz makubwa jana katika mji wa Homs kuwashambulia wanajeshi waliooasi jeshi hilo na kujiunga na wananchi wanaompinga rais Bashar al Assad.