SYRIA

Vikosi vya Syria vya shutumiwa kutekeleza mauaji dhidi ya Raia

vikosi vya Syria
vikosi vya Syria jssnews

Waangalizi wa kimataifa wa maswala ya haki za binaadam wamevishutumu vikosi vya serikali ya Syria kwa utekelezaji wa uhalifu dhidi ya Ubinaadam.

Matangazo ya kibiashara

Katika Ripoti iliyotolewa siku moja kabla ya jumuia ya nchi za Kiarabu kufanya mkutano wao juu ya hali ya Syria,shirika hilo limeitaka jumuia hiyo kuivua uanachama Syria.

Waangalizi hao wameitaka jumuia ya nchi za kiarabu kulitaka baraza la usalama la umoja wa mataifa kuiwekea vikwazo vya marufuku ya kusafirisha silaha na vikwazo dhidi ya maafisa wanaohusika katika machafuko hayo, halikadhalika kuwafikisha katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita.

Ripoti hiyo imetolewa ikizingatia ushahidi wa waathiriwa 110 na mashuhuda huku ikieleza kuwa aina ya ukandamizaji dhidi ya raia wa mjini Homs umejumuisha vitendo vya kutesa na mauaji.

Mauaji ya hivi karibuni yametolewa kwenye Ripoti hiyo ambapo inaelezwa kuwa takriban watu 104 wameuawa tangu tarehe mbili mwezi huu baada ya Raisw wa Syria Bashar Al Assad kutia saini mapendekezo yaliyotolewa na jumuia ya nchi za kiarabu ya kukomesha machafuko nchini humo.