Palestina

Rais wa mamlaka ya wa Palestina kukutana na kiongozi wa Hamas jijini Cairo

Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas
Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas ELECTION

Rais wa mamlaka ya wa Palestina Mahmoud Abbas na kiongozi wa chama cha HAMAS, Khaled Meshaal wanatarajia kukutana Mjini Cairo, nchini Misri tarehe 24 mwezi huu kwa ajili ya mazungumzo ya upatanishi.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo utalenga juu ya kuwepo umoja nchini Palestina,mustakabali wa Palestina, chama cha ukombozi cha Palestina PLO na maendeleo yake.

Chama cha Fatah kilitia saini mchakato wa makubaliano na chama cha Hamas mwezi May ambapo pande hizo mbili zinatarajiwa kuunda serikali ya mpito itakayokuwa na kazi ya kuandaa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika ndani ya mwaka mmoja.

Hata hivyo makubaliano hayo hayakufanyiwa kazi, huku pande hizo mbili zikilumbana juu ya kuundwa kwa serikali ya mpito na juu ya atakayeongoza serikali hiyo.
Abbas amependekeza kufanyika kwa uchaguzi mwezi januari mwakani ili kumaliza mgogoro.