Yemeni

Rais wa Yemen arejelea kauli yake ya

Ali Abdallah Saleh
Ali Abdallah Saleh

Rais wa Yemeni Ali Abdullah Saleh amerejea tena kauli yake ya kuwa tayari kung'atuka madarakani katika kipindi cha siku tisini zijazo baada ya kukamilisha mchakato wa kutoa madaraka kwa wananchi na kusitisha miezi tisa ya machafuko nchini mwake.

Matangazo ya kibiashara

Rais Saleh amesema wameshafikia makubaliano ya kuondoka madarakani ambayo yalifikiwa na mataifa sita wanachama wa Nchi za Ghuba ambayo yanataka Makamu wa Rais Abd-Rabbu Mansour Hadi achukue uongozi wa nchi hiyo kwa sasa.

Uamuzi huo umekuja kwa sasa ikiwa ni mara ya pili baada ya hapo awali Rais Saleh akiwa nchini Saudi Arabia anapatiwa matibabu aliahidi kuondoka madarakani mapema ili kuepusha machafuko na vifo zaidi.