Syria

Nchi za kiarabu zakutana Morocco kuongeza shinikizo kwa Rais Assad kung'oka madarakani

Reuters

Viongozi wa mataifa ya kiarabu wanakutana nchini Morrocco hivi leo, kuzungumzia uongozi wa Syria, ambao unaendelea na mauaji dhidi ya raia wake wanaotaka mabadiliko katika serikali yao. Mkutano huo unafanyika baada ya jumuiya ya mataifa hayo ya kiarabu kuisimamisha Syria uwanachama wake, huku shinikizo za kumtaka rais Bashar Al-Asadd kujizulu zikiendelea.

Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Syria,imesema haitahudhuria mkutano huo jijini Rabat ambao mawaziri hao wa nchi za kigeni wa mataifa wanatarajiwa kuidhinisha rasmi marufuku ya Syria katika umoja huo.

Umoja wa mataifa unasema kuwa, zaidi ya waadamanaji 3500 wamepoteza maisha yao mikononi mwa wanajeshi wa Syria, tangu maandamano yaliponza mapema mwaka huu, huku wengine zaidi ya 70 wakiaga dunia kuanzia mapema juma hili.

Marekani imetaka viongozi hao wa nchi za kiarabu kuongeza shinikizo zaidi kwa rais Bashar Al-Asadd na kumtumia ujumbe wa kumkumbusha kuwa wakati umefika kwa yeye kukubali mabadiliko ya kisiasa nchini humo na kukomesha mauaji dhidi ya waandamanaji.

Mfalme wa Jordan Adullah wa pili amemtaka rais Asaad kujiuzlu,huku waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amasema rais Bashar hana lingine bali kuwasikiliza wananchi wake.