Syria

Ngome kubwa ya kijeshi yashambuliwa nchini Syria

REUTERS

Wanajeshi walioasi jeshi la Syria wameshambulia kambi kubwa ya kijeshi karibu na mji mkuu wa nchi hiyo, Damascus na shambulizi hilo limeongeza wasiwasi wa kutokea kwa mashambulizi zaidi.Taarifa hizo zimetolewa na vikundi vya upinzani nchini humo na kutishia mashambulizi zaidi dhidi ya majeshi yanayomuunga mkono Rais wa Syria, Bashar AL Assad ambaye hata hivyo ameendelea na mpango wake wa kutoondoka madarakani.

Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya sehemu za jengo la jeshi la usalama wa anga mjini Harasta zimehariwa lakini hakukua na taarifa zozote kuhusu vifo au majeruhi.

Shambulizi hilo limetokea huku ukifanyika mkutano wa Muungano wa nchi za Kiarabu nchini Morocco ili kujadili njia za kumaliza mauaji yanayoendelea kutokea nchini Syria huku majeshi yakiendelea kuwashambulia raia waandamanaji wanaopinga utawala wa Bashar Al Assad.

Aidha mkutano huo huenda ukatoka na azimio la kuisimamisha uanachama nchi ya Syria kutokana na hali mauaji ya raia waandamanaji nchini humo.