IRAN

Iran yawanyonga hadi kufa wafanyabiashara wawili wa dawa za kulevya

REUTERS/Eric Thayer

Serikali ya Iran imewanyonga hadi kufa wafanyabiashara wawili wa dawa za kulevya tukio lililofanyika katika Jiji la Qom baada ya ombi lake la kutaka msahama kutupiliwa mbali na mahakama iliyokuwa inasikiliza shauri hilo.

Matangazo ya kibiashara

Kunyongwa kwa watu hao wawili kunakuja ukiwa ni muendelezo wa matukio ya kutekeleza adhabu ya kifo ambayo imekuwa ikitekelezwa nchini Iran kwa wale wenye makosa ya ubakaji, wizi wa kutumia silaha na biashara ya dawa za kulevya.

Idadi ya watu ambao wameshakambana na adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa mujibu wa serikali ya Iran imefikia watu mia mbili na arobaini na tatu huku takwimu za Shirika la Kutetea Haki za Binadamu zikionesha watu mia tatu na themanini na nane walinyongwa mwaka 2010.

Dawa za kulevya zimekuwa zikipigwa vita na kila nchi lakini bado limekuwa ni tatizo ambalo linaathiri nchi nyingi zikiwemo nchi za Bara la Afrika.

Matumizi ya dawa za kulevya yanawaathiri zaidi vijana na yamekuwa yakitajwa kama chanzo cha maambukizi ya Ukimwi.