Syria

Mataifa ya kiarabu yatoa siku tatu kwa Rais Assad kumaliza mauaji

Reuters/Stringer

Mataifa ya nchi za kiarabu yamempa rais wa Syria Bashar Al-Assad siku tatu kumaliza mauaji dhidi ya waandamanaji nchini humo, wanaotaka mabadiliko ya kisiasa nchini mwake. Mawaziri wa nchi za kigeni wa mataifa hayo ya kiarabu wamesema kuwa, ikiwa rais Bashar hatasitisha mauaji hayo, Syria itapata vikwazo zaidi kutoka kwa muungano wa mataifa hayo.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano wa mawaziri wamekutana mjini Rabat nchini Morocco na kushutumu uongozi wa Assad kwa kuendelea kuwagandamiza wanadamanaji ambao wanataka mabadiliko ya kisiasa nchini humo.

Syria inazidi kutengwa na jumuiya ya kimataifa, baada ya mataifa mbali mbali kutishia kuwarudisha nyumbani mabaliozi wake mjini Damascus, huku Morocco ikimrudisha nyumbani balozi wake huku Ufaransa ikisema itamrudisha balozi wake nyumbani.

Mwishoni mwa juma lilipota muungano wa nchi hizo za kiarabu uliisimamasiaha Syria, kuwa mawanachama wake kutokana na mauaji makubwa ya wanadamanaji.

Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, zaidi ya wanadamaji 3,500 wameuawa tangu maandamanao hayo yalipoanza mapema mwaka huu.