SYRIA-UTURUKI

Wanajeshi wa Syria watuhumiwa kushambulia msafara wa mahujaji wa Uturuki wakitokea Saudi Arabia

Raia mmoja wa Uturuki amekufa na wengine zaidi ya watano wamejeruhiwa vibaya kufuatia basi walilokuwa wakisafiria kushambuliwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni wanajeshi wa Syria jirani na mpaka wa nchi hiyo na Uturuki.

Waziri mkuu Racep Erdogan alipkutana hivi karibuni na rais wa Syria Bashar al-Asad
Waziri mkuu Racep Erdogan alipkutana hivi karibuni na rais wa Syria Bashar al-Asad Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kituo cha televisheni nchini Uturuki kimeripoti basi hilo kuvamiwa na kushambuliwa na wanajeshi hao likiwa katika kituo cha ukaguzi muda mfupi kabla ya basi hilo lililokuwa limewabbea mahujaji waliotoka Macca kuingia nchini Uturuki.

Basi hilo ni moja kati ya mabasi matatu ambayo yalikuwa yamewabeba mahujaji raia wa Uturuki waliokuwa wakitokea nchini Saudi Arabia walikokuwa wamekwenda kufanya haji.

Tukio hilo limeonekana kuwashtua watu wengini nchini Uturuki akiwemo waziri mkuu Racep Tayyip Erdogan ambaye ametoa onyo kali kwa serikali ya Syria dhidi ya kitendo hicho akitishia kuvunja uhusiano wake kabisa na nchi hiyo.

Licha ya shinikizo toka jumuiya ya kimataifa, majeshi ya Syria yameendelea kusalia katika miji mbalimbali nchini humo yakiendesha operesheni za kuwakamata wanaharakati wanaohamasisha maandamano nchini humo.

Shambulio hilo linakuja wakati ambapo viongozi wa Umoja wa nchi za Kiarabu wanakutana kujadili hatma ya uanachama wa Syria kufuatia makataa waliyoitoa juma moja lililopita kwa nchi ya Syria kusitisha mauaji dhidi ya raia kupita.