YEMEN-SAUD ARABIA

Rais wa Yemen awasili Saudi Arabia kwaajili ya kutia saini makubaliano ya kukabidhi madaraka kwa makamu wake

Rais wa Yemen Ali Abdulah Saleh
Rais wa Yemen Ali Abdulah Saleh Reuters

Rais wa Yemen Ali Abdulah Saleh amewasili nchini Saudi Arabia kwa mwaliko wa Serikali ya mfalme Abdulah ambapo rais huyo anatarajiwa kutia saini makubaliano ya kuachia madaraka kwa makamu wake.

Matangazo ya kibiashara

Rais Saleh aliwasili katika uwanja wa Riadh na kulakiwa na wenyejei wake ambapo baadae anatarajiwa kufanya mazungumzo na mfalme Abdulah kabla ya kukubali kutia saini makubaliano hayo.

Nchi za kiarabu za Ghuba miezi michache iliyopita walifanya mazungumzo na Serikali ya rais Saleh ambapo walikubaliana kiongozi huyo akubali kutia saini hati ya kukabidhi madaraka kwa makamu wake ambapo atakuwa na kinga ya kutoshtakiwa.

Rais Saleh mara kadhaa amekuwa akisisitiza kuwa atatia saini makubalinao hayo endapo atahakikishiwa usalama wake ikiwa ni pamoja na kutoshtakiwa yeye na familia yake endapo atakabidhi madaraka kwa makamu wake wa rais Abdrabuh Mansur Hadi ambaye ataongoza kupatikana kwa Serikali ya mpito.

Hata hivyo haijabainika endapo kiongozi huyo atatia saini makubaliano hayo au la kwa kile kilichoelezwa hii itakuwa sio mara ya kwanza kwa kiongozi huyo kusema atatia saini makubalinao hayo na kisha asifanye hivyo.

Kumekuwa na maaandamano yanayoendelea katika miji mbalimbali nchini humo kwa wananchi kushinikiza kujiuzulu kwa rais Saleh.