Afghanistan

Marekani kufanya Uchunguzi juu ya Mauaji ya Raia wa Afghanistan yaliyofanywa na Mwanajeshi wa Marekani

Rais wa Marekani Barrack Obama
Rais wa Marekani Barrack Obama REUTERS/Jason Reed

Marekani imeahidi kufanya uchunguzi juu ya hatua ya mwanajeshi wake,kuwaua Raia 16 wa Afganistan kwa kuwapiga risasi siku ya jumapili juma lililopita, hali ambayo imezidisha hali ya wasiwasi baada ya kuchomwa Kitabu cha kuran tukufu.

Matangazo ya kibiashara

Rais Obama ametoa salamu za Rambirambi kwa serikali ya Afghanistan pamoja na kwa Familia zilizopatwa na mkasa huo alioeleza kuwa wa kushangaza na kusema uchunguzi unafanyika na hatua zitachukuliwa dhidi ya mwanajeshi huyo.
 

Mwanajeshi huyo alitekeleza mauaji hayo ya watoto 9 na wanawake kusini mwa mkoa wa Kandahar.
 

Ubalozi wa Marekani mjini Kabul umetoa tahadhari kwa Raia wa Marekani walio nchini Afghanistan kuwa kufuatia mauaji hayo kutakuwa na madhara ya kuwepo kwa chuki dhidi ya Marekani na maandamano siku zijazo.

Mashambulzi haya yanatikisa uhusiano wa kidilpkmasia katia ya Mareakani na Afganistan na rais Hamid Karzai amekashifu kitendo hicho na kutaka ufafanuzi kutoka kwa Marekani kutokana na mauji hayo.