SYRIA

Waangalizi wa Umoja wa mataifa UN wawataka raia kutoshiriki maandamano

Raia nchini Syria wakiwa katika maandamano kuushinikiza utawala wa raisi Assad kuondoka madarakani
Raia nchini Syria wakiwa katika maandamano kuushinikiza utawala wa raisi Assad kuondoka madarakani REUTERS

Melfu ya raia wa syria wameandamana kwenye miji mbalimbali nchini humo wakishinikiza kujiuzulu kwa raisi Bashar al Assad na utawala wake ambao bado umeendelea kusalia madarakani.

Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo yamefanyika wakati bado waangalizi wa umoja wa mataifa UN wakiwataka wananchi kutoshiriki maandamano yoyote ambayo yanaweza kuleta ghasia na kutishia usalama.

Naye msemaji wa msuluhishi wa mgogoro wa Syria Koffi Annan Ahmad Fawzi amesema kuwa bado kuna mapendekezo hayajafanyiwa kazi na pande zote mbili zinazokinzana kwakuwa bado kuna baadhi ya silaha zinaendelea kumilikiwa na wapiganaji wa jeshi huru.

Maelfu ya raia nchini Syria wameendelea kupoteza maisha tangu kuzuka kwa machafuko nchini humo mwaka jana,ambapo raia wamekuwa wakipambana na majeshi ya serikali ya raisi Assad wakimtaka aachie madaraka.