Syria

Kundi Jipya laibuka Nchini Syria ladai li tayari kupambana na Serikali ya Nchi hiyo

Moja ya mashambulizi ya bomu yaliyotekelezwa nchini Syria
Moja ya mashambulizi ya bomu yaliyotekelezwa nchini Syria Reuters

Kundi jipya limeibuka nchini Syria linalotambulika kwa jina la Al Nusra likijiapiza kuwa tayari kupambana na serikali ya Rais Bashar Al Assad wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa UN ukiendelea kupigana kuhakikisha wanapata suluhu ya umwagaji damu nchi humo.

Matangazo ya kibiashara

Kundi la Al Nusra limejitokeza na kutuma video zao zinazoonesha namna ambavyo wanafanya mazoezi na kueleza wameshatekeleza mashambulizi kadhaa ya kujitoa mhanga nchini Syria wakieleza nia yao nio kuanzisha Jihadi dhidi ya serikali.
 

Taarifa za kuibuka kwa Kundi jipya zinakuja wakati huu ambapo Wangalizi wa Umoja wa Mataifa UN wapatao mia moja na themanini na tisa wakiwa nchini Syria kujionea hali ilivyo na hapa Mkuu wao Meja Jenerali Robert Mood anasema wananchi wanaimani nao.
 

May 10 mashambulizi mawili ya mabomu yaligharimu maisha ya watu 55 jijini Damascus na wengine 372 kujeruhiwa mashambulizi yanayoelezwa kuwa na madhara makubwa zaidi tangu kuzuka kwa harakati za Maandamano ya kuangusha utawala wa Rais wa Syria Bashar Al Assad yaliyoanza Mwezi March mwaka 2011.