Palestina-Israel

Wafungwa wa Kipalestina kusitisha mgomo baada ya ahadi ya kusikilizwa matakwa yao

Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu
Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu REUTERS/Gali Tibbon/Pool

Kamati maalumu iliyoundwa kushughulikia mzozo wa wafungwa wa kipaletsina walioko kwenye magereza ya nchini Israel wakiwa kwenye mgomo wa kula imesema kuwa wamefanikiwa kufikia makubaliano kwa wafungwa hao kusitisha mgomo wao. 

Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo kati ya viongozi wa Israel na Palestina yalikuwa yanafanyika nchini Misri ambapo kiongozi wa magereza nchini Palestina Issa Karaka amethibitisha pande hizo mbili kufikia muafaka.

Moja ya mambo ambayo wamekubaliana ni kwa serikali ya Israel kuwafungulia mashtaka rasmi wafungwa wanaowashikiliwa ili kuharakisha kesi zao pamoja na kuruhusu wafungwa hao kutembelewa na ndugu zao wakiwa kizuizini.

Wafungwa wakipalestina wanaoshikiliwa na mamlaka nchini Israel wameendelea kuwa kwenye mgomo wa kula kwa siku zaidi ya sabini wakishinikia kufunguliwa mashtaka.

Takriban Wafungwa wa kipalestina 1550 hivi sasa wako kwenye Mgomo, wawili kati yao wamefikisha siku ya 76 ya Mgomo wa kutokula.

Madai ya Wafungwa hao ni pamoja na kuhitaji kuziona Familia zao, kupatiwa Elimu, kupatiwa wanasheria wa kutosha, kutotengwa na kutoshikiliwa bila kufunguliwa Mashtaka.