Pakistani

Pakistani kufungua mipaka yake kwa Majeshi ya NATO

Rais wa Pakistan Asif Ali Zardari
Rais wa Pakistan Asif Ali Zardari

Pakistan hii leo inatazamia kuondoa marufuku dhidi ya vikosi vya jumuia ya kujihami ya Nchi za Magharibi, NATO vikosi ambavyo vilikoma kusambaza misaada baada ya Pakistan kufunga mipaka yake.

Matangazo ya kibiashara

Islamabad ilifunga mipaka baada ya shambulio la anga lililotekelezwa na vikosi vya Marekani kugharimu maisha ya wanajeshi 24 Mwezi November mwaka jana na kusababisha uhusiano kati ya mataifa hayo kutetereka, hali iliyojitokeza kama ya baada ya kuuawa kwa kiongozi wa Wanamgambo wa Al Qaeda, Osama Bin Laden.
 

Hii leo, viongozi wa Kiraia na Kijeshi wanakutana kujadili juu ya kufungua tena njia za usafirishaji katika mkutano wa Kamati ya Baraza la Ulinzi, na baadae mkutano wa wakuu wa Baraza.
 

Vyanzo vya Habari vimeliambia shirika la Habari la Ufaransa, AFP kuwa Serikali imeamua kufungua Mipaka yake na kuwa huenda utekelezaji ukaanza mwanzoni mwa juma lijalo, na kuwa kuna matumaini kuwa Nchi hiyo itaalikwa kwenye mkutano wa NATO utakaofanyika jijini Chicago nchini Marekani May 20 mpaka tarehe 21.
 

Pakistan imeitaka Marekani kutotekeleza mashambulio ya anga yanayolenga wanamgambo wa Taliban na Al Qaeda katika ardhi yake.
Kujihusisha kwa Pakistan katika mkutano wa Chicago kutapunguza hali ya kutengwa na jumuia ya kimataifa.