Syria

Vikosi vya Syria vyashutumiwa kutekeleza mauaji ya Raia 15 nchini humo

Rais wa Syria Bashaar Al Assad
Rais wa Syria Bashaar Al Assad Reuters/Benoit Tessier

Vikosi vya Syria vimeshutumiwa kwa kutekeleza mauaji ya Raia 15 wakati huu ambapo Timu ya waangalizi wa Umoja wa Mataifa wakiondoka mji ulimotokea shambulio la Bomu dhidi yao.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Syria Bashar Al Assad, hata hivyo ameyashutumu Mataifa ya Magharibi kwa kupuuza machafuko yanayosababishwa na kile alichodai Magaidi na kusema kuwa atahitaji maelezo kutoka kwa Msuluhishi wa Mgogoro wa Nchi hiyo kutoka UN Koffi Annan atakapotembelea Damascus baadae Mwezi huu.

Umoja wa Mataifa ambao umekuwa ukizisihi pande mbili nchini Syria kuacha mapigano, umelaani Mashambulizi yeyote dhidi ya Waangalizi wa Umoja huo walio nchini humo.
 

Shirika linalotetea haki za Binaadam la nchini Syria limeshutumu vikosi vya Serikali kwa mauaji katika mji wa Khan Sheikhun, na mjinni Idlib, baada ya kushambulia watu waliokuwa wakiendelea na shughuli za Mazishi, shambulio linaloelezwa kuwa watu 20 walipoteza maisha.

Annan mwenyewe ameeleza kuwa mchakato wa utekelezaji wa Mapendekezo unachukua muda mno na ameitaka Syria kutopuuza Makbaliano ya utekelezaji wa makubaliano halikadhalika kuruhusu Umoja huo kuwafikia zaidi ya Raia wa Syria milioni moja wanaohitaji msaada.