Syria

Vikosi vya Syria vyawafyatulia Risasi Raia walioandamana katika Miji kadhaa nchini humo

Rais wa Syria Bashaar Al Assad
Rais wa Syria Bashaar Al Assad

Vikosi vya nchini Syria vimewafyatulia Risasi Raia  walioandamana katika Mitaa mbalimbali Mjini Aleppo hii leo na kujeruhi watu kadhaa katika maandamano makubwa mjini humo. 

Matangazo ya kibiashara

Shirika linalotetea haki za Binaadam nchini humo limesema kuwa waandamanaji pia wamejeruhiwa katika mji wa Douma, mji ulio kiini cha maandamano.

Miji mingine yalikofanyika maandamano nchini Syria ya kutaka kuondoka kwa utawala wa Rais wa nchi hiyo, Bashar Al Assad ni Damascus, Deir Ezzor, Homs na kaskazini magharibi mwa Idlib.

Maelfu ya Watu waliandamana katika Maeneo mbalimbali Mjini Aleppo ingawa kumekuwepo na vizuizi kutoka kwa Utawala wa nchi hiyo.

Serikali ya Syria imesema kuwa vikosi vyake vilizuia shambulio la bomu la kujitoa muhanga Mjini Aleppo ijumaa juma lililopita, siku moja baada ya Shambulio la bomu kuuua watu 55 jijini Damascus na kujeruhi wengine takriban 400 na kusisitiza kuwa matukio hayo yanatekelezwa na Magaidi.
 

Hapo jana Wanafunzi mbalimbali walikutana huku wakizuiwa na vikosi vya usalama mbali na uwepo wa waangalizi wa Umoja wa Mataifa ambao hivi sasa wako zaidi ya 250 nchini kote.