Yemeni

Makundi ya misaada yaonya kuhusu hatari ya Yemeni kupungukiwa chakula

AFP/ MOHAMMED HUWAIS

Makundi saba ya misaada yametoa angalizo kwa wanadiplomasia wa magharibi kuwa Yemen iko kwenye hatari ya kupungukiwa chakula na kuwataka kuongeza juhudi ili kunusuru hali hiyo wakati huu wanadiplomasia hao wanapotarajia kukutana Mjini Riyadh kwa ajili ya mkutano wa kimataifa unaolenga kuisaidia Yemen.

Matangazo ya kibiashara

Mashirika ya Oxfam, CARE na Save the Children yameeleza uwepo wa hali hiyo huko yemen katika taarifa iliyotolewa hii leo wakati ambapo marafiki wa Yemen wakitarajia kukutana.

Imeelezwa kuwa katika takriban watu milioni 10, asilimia 44 ya watu wote hawapati chakula cha kutosha, na mtoto mmoja kati ya watatu ana tatizo la utapiamlo.

Mkurugenzi wa OXFAM nchini Yemen, Penny Lawrencde amesema kuwa familia mbalimbali za Raia wa Yemen zimeingia katika madeni wakiwa katika juhudi za kulisha familia zao.

Lawrence amesema nchi zinazosaidia Yemen katika suala la siasa na usalama ambao umeendelea kuwa wa hofu kwa maendeleo ya Yemen, zitakuwa zinafanya kazi bure iwapo zitashindwa kutafuta suluhu ya haraka kwa uhitaji wa missada ya kibinaadam hali itakayofanya maisha ya Raia wa Yemen kuwa hatarini.