Syria

Rais Bashar Al Assad asema Serikali yake ina uwezo wa kutatua mgogoro

Serikali ya Syria imesema kuwa bado inaweza kushughulikia mgogoro unaosumbua nchi hiyo kwakuwa ina uzoefu katika kupambana na vitisho na mashinikizo mbalimbali ambayo yamewahi kutokea kwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

 

Raisi wa Syria Bashar al-Assad amesema hayo alipokutana na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia kutoka Iran, Reza Taqipour ambaye alifika Syria kwa niaba ya raisi wa Iran Mahmoud Ahmednejad.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Syria Waziri Taqipour alifika kumwalika Raisi Assad katika mkutano wa nchi zisizofungamana na upande wowote utakaofanyika mwezi wa tisa huko Tehran.

Waziri Taquor amesema kuwa serikali yake inaunga mkono wana Syria katika kukabiliana na mgogoro nchini mwao.

Mualiko huo unakuja wakati kundi la waasi nchini Syria linaituhumu Iran kuisaidia mamlaka ya Syria katika kuchangia machafuko ambayo yamedumu kwa kipindi cha miezi 14 na kugharimu maisha ya watu takribani 12,600 kwa mujibu wa waangalizi.