Syria

Vikosi vya Serikali ya Syria vyawafyatulia risasi waandamanaji 1,500

Reuters

Vikosi vya usalama nchini Syria vimewafyatulia Risasi wandamanaji takriban 1500 waliokuwa wakiwakumbuka wanafunzi wanne wa chuo cha Allepo waliouawa na vikosi vya usalama wakati wa maandamano tarehe 3 mwezi huu.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo dhidi ya waandamanaji lilisababisha mapigano kati ya kundi la upinzani lenye silaha la Free Syrian Army FSA na vikosi vya Syria mapigano yaliyofanyika mjini Allepo.

Wakati huu ambapo mapigano yameendelea kupamba moto, mmoja kati ya washirika wa Syria, Urusi imesema itafanya mazungumzo ya moja kwa moja na utawala wa Syria na wawakilishi wa waasi nchini humo, Naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Mikhail Bogdanov amethibitisha.

Katika hatua nyingine Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo Burhan Ghaliun amejiuzulu wadhifa wake taarifa kutoka baraza la taifa nchini Syria zimethibitisha.

Ghaliun halikadhalika ametoa wito wa kuachiwa huru kwa waumini wa Kishia akiwa na imani kuwa utawala wa Syria umehusika katika kutekwa nyara kwa Walebanon hao.