Bahrain

Mahakama ya Rufaa nchini Bahrain yatupilia mbali rufaa ya Wanaharakati

Mfalme Hamad Al-Khalifa wa Bahrain
Mfalme Hamad Al-Khalifa wa Bahrain Reuters/Stephanie McGehee

Mahakama kuu ya Rufaa nchini Bahrain imetupilia mbali Rufaa iliyokatwa na Viongozi kumi na watatu wa upinzani ambao walihukumiwa adhabu tofauti ikiwemo kifungo cha maisha jela kwa kosa la kutaka kupindua Serikali.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama hiyo imetupilia mbali rufaa ya mwisho ya Viongozi ambao wanatajwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha Utawala uliokuwa madarakani nchini Bahrain unang'olewa kupitia maandamano ambayo yaliandaliwa na Wanaharakati.
 

Miongoni mwa Viongozi hao wapo Wanaharakati Adulhadi Khawaja ambaye alifunga kula na kunywa kwa siku 110 akipinga adhabu ya kifungo cha maisha Jela iliyotolewa na mahakama.
 

Wanaharakati saba kati ya kumi na watatu watalazinika kutumikia kifungo cha maisha jela akiwemo Khawaja, Hassan Mashaima ambaye ni Kiongozi wa kundi la Haq na Aduljalil Al Singace ambaye ni Mwanachama.
 

Wanaharakati hao ambao ni wapinzani nchini Bahrain walisimama kidete kwenye maandamano ya Mwaka 2011 yaliyokuwa yakishinikiza kubadilishwa utawala ambapo watu 80 walipoteza maisha kwenye mapambani na Polisi.