Syria

Rais Assad wa Syria ahutubia Raia nchini mwake akituhumu Mataifa ya kigeni kuingilia maswala ya Syria

Rais wa Syria, Bashar Al Assad
Rais wa Syria, Bashar Al Assad REUTERS/Syrian TV via Reuters TV

Hotuba ya Rais Bashar Al Assad akitoa wito wa kuwepo kwa amani nchini humo imekumbana na ukosoaji mkubwa na upande wa upinzani na kimataifa, huku Iran pekee ikiunga mkono msimamo wake.

Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya Mkuu wa sera za mambo ya nje ndani ya Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton imesema kuwa msimamo wa Ulaya unaendelea kumtaka Assad kuondoka madarakani ili kupisha mchakato wa kufanyika mabadiliko ya kisiasa.
 

Iran pekee inayotoa msaada wa kifedha, washauri wa maswala ya kijeshi na kwa mujibu wa Marekani Silaha kwa utawala wa Assad imempongeza Assad na kutangaza kumuunga mkono katika harakati zake za kumaliza machafuko nchini Syria.
 

Katika Hotuba yake ya kwanza kwa kipindi cha miezi saba, hapo jana alieleza mipango yake katika kuhakikisha mgogoro wa miezi 21 uliokumba nchi hiyo na kuua watu zaidi ya 60,000 kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa.
 

Assad amesema kuwa Maazimio yoyotea ya kumaliza mzozo nchini mwake ni budi yakawahusu Raia wenyewe na kushutumu kuwa wanaompinga si wapinzani isipokuwa makundi ya wauaji akidai kuwa wageni kutoka nje wenye mtazamo wa kundi la wanamgambo wa Al Qaeda.