Syria

Mapigano yapamba Moto nchini Syria katika Makazi ya Wakurdi

Rais wa Syria, Bashar Al Assad
Rais wa Syria, Bashar Al Assad AFP PHOTO/SYRIAN TV

Mapigano makali yamezuka hapo jana Mjini Ras al-Ain kaskazini mwa Syria katika eneo lenye makazi ya Wakurdi katika eneo la mpaka wa nchi hiyo na Uturuki.

Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo yamekuja ikiwa ni miezi sita baada ya Vikosi vinavyomtii Rais wa nchi hiyo, Bashar Al assad kuondoka katika maeneo wanayoishi Wakurdi, wakiwaacha Raia kujilinda wenyewe.

Wapiganaji wamefanya mashamulizi kadhaa katika mji huo na kusababisha Raia wengi kukimbia mji huo.

Wakkurdi waishio nchini Syria wamegawanyika kwa makundi ya wanaunga mkono na wanaompinga Rais Assad huku wengine wakiwa hawaegemei upande wowote.

Katika hatua nyingine, Raia 100 wameuawa nchini humo Taasisi inayotetea haki za binaadam imeeleza hapo jana wakati urusi ikioneah kutokubaliana na shutma za Marekani iliyodai Serikali ya Damascus kuhusika na Mashambulizi ya Mabomu katika chuo kikuu cha Aleppo.