Syria

Marekani yatangaza kusaidia Waasi wa nchini Syria

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry REUTERS/Jacquelyn Martin/Pool

Marekani imetangaza kuwa itatoa msaada wa Dola Milioni 60 kwa muungano wa upinzani nchini Syria kuwasaidia kuweka mikakati ya kupata suluhu la kisiasa na kuunagisha uongozi wa rais Bashar Al Assad.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani katika kikao na viongozi wa upinzani wa Syria mjini Rome nchini Italia ameongeza kuwa serikali yake pia itatoa msaada wa chakula na huduma za matibabu kwa muungano huo wa upinzani.

Hatua hiyo imeelezwa kuwa muhimu hata hivyo imeelezwa kuwa haikidhi haja ya Waasi hao ambao wamekuwa wakihitaji kupatiwa silaha.

Hatua hiyo iliyoatangazwa na Waziri wa mambo ya nje wa Mareakani, John Kerry imelenga kuupa upinzani uwezo wa kudhibiti maeneo wanayoyashikilia kutoka kwa Utawala wa Syria.
 

Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa hatua hii ya Marekani ni kujiingiza ndani zaidi kwenye Vita vya nchi hiyo kwa kukubali kuwapa Waasi msaada wa moja kwa moja, huku wengine wakisema kuwa misaada hiyo imechelewa.