ISRAEL

Netanyahu apewa majuma mawili zaidi kuunda serikali mpya

Raisi wa Israel Shimon Peres
Raisi wa Israel Shimon Peres DR/haaretz.com

Raisi wa Israel Shimon Peres amemtaka waziri mkuu wake Benjamin Netanyahu kukamilisha zoezi la kuunda serikali mpya ndani ya majuma mawili baada ya kushindwa kutekeleza agizo hilo katika majuma mawili ya awali.

Matangazo ya kibiashara

Hayo yanakuja baada ya orodha ya chama chake cha Likud-Beitenu kuibuka kama chama kikuu katika uchaguzi wa mwezi january 22 na kushinda viti 31,mapema tarehe mbili february Natanyahu alikabidhiwa jukumu rasmi la kuunda serikali ya muungano.

Awali Raisi Peres alimtaka waziri Nyatanyahu kukamilisha jukumu lake ndani ya siku 28 kwa mujibu wa sheria.

Ikiwa muda wa nyongeza utakwisha bila Nyatanyahu kukamilisha jukumu hilo raisi Peres atalazimika kumuagiza mbunge mwingine kujaribu kutekeleza jukumu hilo la kuunda serikali mpya.