SAUDI ARABIA

Marekani kuendelea kuwasaidia wapinzani nchini Syria

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry nydailynews.com

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kery amefanya mazungumzo na washirika wake kutoka mataifa sita ya ghuba ya falme za kiarabu kuhusu vita nchini Syria na mpango wa nyuklia wa Iran, ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu apate wadhifa huo. 

Matangazo ya kibiashara

Kerry, ambaye ameawasili katika mji mkuu wa Saudi Jumapili jioni baada ya ziara ya siku mbili jijini Cairo nchini Misri, ameanza kwa kufanya mkutano majira ya asubuhi na mawaziri wa nje wa Bahrain na Kuwait. ambapo amesema kuwa Marekani na washirika wake itaendelea kuwasaidia wapinzani nchini Syria.

Hapo baadaye Kerry anatarajia kufanya mazungumzo na mawaziri wa kigeni wa mataifa mengine manne yanayounda baraza la muungano la Ghuba (GCC) ambazo ni Saudi Arabia, Falme za Kiarabu, Oman na Qatar.

Aidha afisa wa Idara ya Ikulu ya Marekani amewaambia waandishi wa habari kwamba Kerry pia anataraji kufanya mazungumzo na rais wa Palestina Mahmud Ababas huko Riyadh, katika mkutano ulopangwa kufanyika wakati wa chakula cha mchana.