SYRIA

Assad atamba kubaini njama dhidi ya serikali yake

Rais wa Syria Bashar Al Assad amesema kuwa serikali yake imeshinda njama zilizopangwa dhidi yake hata wakati huu ambapo waasi wamevamia mji mkuu wa jimbo la Raqa na kumteka gavana wake katika hatua kubwa ya mafanikio tangu kuanza kwa harakati zao.

Rais wa Syria Bashar al Assad
Rais wa Syria Bashar al Assad uncyclopedia.wikia.com
Matangazo ya kibiashara

Maoni hayo ya rais Assad yaliyochapishwa leo Jumanne katika gazeti la Al-Akhbar, pia yamebainisha kuwa wapinzani wake, wanaoungwa mkono na mataifa yenye nguvu duniani,walikuwa wakicheza mchezo wa kuwania ushindi ambapo majeshi yake yamekuwa yakishinda katika viwanja vya mapambano.

Aidha gazeti hilo limemkariri rais Assad akiwaambia washirika wake waliomtembelea kutoka uarabuni kuwa, mafanikio muhimu yamefikiwa, ambayo umuhimu wake uko wazi hata kwa wale waliomo ndani ya Syria na sehemu zilizosalia duniani ambao wanafanya mipango isiyo na faida dhidi ya usalama wa Syria.

Utawala wa Assad mara nyingi umeonekana kama uasi uliozuka nchini Syria mnamo mwezi Machi mwaka 2011, kama sehemu ya njama zilizopangwa na mataifa ya kigeni dhidi ya nchi hiyo, huku ikikataa kuitambua serikali.