Hatimaye Benjamin Netanyahu afikia makubaliano ya kuunda serikali ya muungano
Hatimaye Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amefikia makubaliano ya kuunda serikali ya muungano kati ya vyama vingine vya siasa na chama chake cha mrengo wa kulia. Makubaliano hayo yamefikiwa siku tatu kabla ya siku ya mwisho aliyopewa ya machi 16 ambayo Netanyahu alitakiwa kutangaza serikali mpya.
Imechapishwa:
Sherehe za kusaini makubaliano ya kuunda serikali hiyo zinatarajiwa kufanyika alhamisi hii na serikali mpya inatarajiwa kuanza kazi juma lijalo kabla ya Rais wa Marekani Barack Obama kuzuru katika Taifa hilo.
Mazungumzo pamoja na vyama vinavyotegemewa kuunda serikali ya muungano nchini Israel yalikiuwa yakikwama mara kadhaa na kumfanya Netanyahu kuomba muda zaidi ili kuepuka kuitishwa kwa uchaguzi mwingine ambao huenda ungemuangusha zaidi.
Katika uchaguzi wa mwezi januari 22 muungano wa vyama vilivyoongozwa na Benjamin viliongoza kwa kupata viti 31 kati ya viti vyote 120 vya bunge la nchi hiyo na hivyo kuwa na haki ya kumteua Waziri Mkuu.