SYRIA

Marekani kuongeza mara mbili zaidi msaada wake kwa wapinzani nchini Syria.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani,John Kerry
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani,John Kerry RFI

Marekani imesema kuwa itaongeza mara mbili misaada yake kwa upinzani nchini Syria, ikiwa ni pamoja na vifaa vipya vipya vya kijeshi visivyo vya maangamizi, bila kujali wito wa kuuza silaha au kuingilia moja kwa moja. 

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake baada ya mazungumzo kati ya marafiki wa Syria wanaounga mkono upinzani wanaokutana huko Istanbul, waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry alisema msaada wa Marekani kwa upinzani itakuwa ni dola milioni 250 .

Hapo jana Muungano wa upinzani nchini Syria uliikosoa urusi na kusema kuwa imeachwa kando na historia kwa kuunga mkono serikali ya rais Bashar al Assad na kwamba inajitenga yenyewe katika uwanda wa kimataifa.