Marekani

Serikali ya Syria yashutumiwa kutumia Silaha za Kemikali kupambana na Waasi nchini humo

Rais wa Syria, Bashar Al Assad
Rais wa Syria, Bashar Al Assad

Serikali ya Marekani imesema kuna ushahidi unaonesha Rais Bashar Al Assad na Jeshi lake huko Syria wanatumia silaha za kikemikali katika mapambano yao dhidi ya Wapinzani ambao kwa zaidi ya miaka miwili wanataka kuiangusha serikali yake.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Chuck Hagel ndiye ametoa kauli hiyyo na kusema wamekusanya usahidi unaothibitisha uwepo wa matumizi ya silaha za kikemikali uliofanywa na Taasisi zao za Kijasusi.

Seneta John McCain amesema kutokana na uwepo wa ushahidi huo ni vyema sasa nchi hiyo ikawasaidia Wapinzani kuiangusha serikali iliyopo madarakani kama ambavyo Rais barack Obama alivyoahidi awali.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron amesema kuwa ushahidi ambao umekuwa ukizidi kutolewa juu ya matumizi ya Silaha za kemikali yanayodaiwa kufanywa na utawala wa Syria ni wa kuogofya kwa jumuia ya kimataifa, huku akiunga mkono Kauli ya Rais Obama ya kuwasaidia Waasi.

Umoja wa Mataifa UN unatarajiwa kupeleka wataalam wake nchini Syria kufanya uchunguzi kubaini kama kweli kuna matumizi hayo lakini wameshindwa kiufanya hivyo kutokana na kusubiri ruhusa ya Serikali ya Damascus.