YEMEN

Wanajeshi 5 wa Yemen wauawa na kundi la kigaidi la Al Qaeda

Baadhi ya wapiganaji wa kundi la kigaidi la Al qaeda,nchini Yemen.
Baadhi ya wapiganaji wa kundi la kigaidi la Al qaeda,nchini Yemen. AFP

Kundi la kigaidi la Al-Qaeda linatuhumiwa kuwaua wanajeshi watano wa jeshi la Yemen katika shambulio lililotokea huko kusini magharibi mwa mji wa sanaa.  

Matangazo ya kibiashara

Mapema ijumaa wizara ya mambo ya ndani nchini Yemen ilisema imechukua hatua za tahadhari kufuatia taarifa za kiintelijensia za kuwepo kwa mashambulizi ya kigaidi kutoka kwa kundi la al qaeda hatua ambayo haikuzuia mashambulizi hayo yaliyolenga kituo cha jeshi wilaya ya Rada.

Maafisa wa serikali wamethibitisha kuuawa kwa wanajeshi watano na wengine kujeruhiwa.

Katika mtandao wa wizara ya ulinzi nchini humo taarifa zimebainisha kuuawa kwa wapiganaji wawili wa al qaeda.