Misri

Chama cha Muslim Brotherhood nchini Misri chadai Wafuasi wake 34 wameuawa na Jeshi la nchi hiyo

Rais wa Misri, Mohamed Morsi, aliyepinduliwa na Jeshi
Rais wa Misri, Mohamed Morsi, aliyepinduliwa na Jeshi Egypt's President Mohamed Mursi reviews the troops at an offici

Takriban Watu 34 wameuawa baada ya kuwepo Mapigano makali kati ya Vikosi vya kijeshi nchini Misri na Waandamanaji walio wafuasi wa Chama cha Muslim Brotherhood jijini Cairo.

Matangazo ya kibiashara

Vyanzo vya kitabibu nchini humo vimesema Watu 16 wameuawa, lakini Chama hicho kimedai kuwa Wafuasi wake 34 wamauawa katika mashambulizi ya Risasi.
 

Jeshi limedai kuwa kundi la kigaidi lilikuwa likijaribu kushambulia eneo ambalo linaloripotiwa kuwa, aliyekuwa Rais wa Misri, Mohamed Morsi anashikiliwa humo.
 

Katika hatua nyingine, Chama cha Al- Nur hii leo kimetangaza kujiondoa kwenye mazungumzo juu ya kuundwa kwa Serikali mpya kwa kile walichodai kutokana na hali ya sasa na Mauaji dhidi ya Waandamanaji wanaotoa wito wa kumrejesha Morsi madarakani.
 

Chama cha Al-Nur, kilichojinyakulia karibu Robo ya Kura za Bunge katika uchaguzi wa mwaka 2011 kiliunga mkono kuondolewa kwa Morsi Madarakani.
 

Wafuasi wa Chama cha Muslim Brotherhood wamejikusanya kwa wingi katika maeneo mbalimbali jijini Cairo siku za karibuni, wakiapa kumtetea Morsi aliyepinduliwa na Jeshi baada ya maandamano makubwa yaliyoshinikiza kuondolewa Madarakani.