ISRAEL

Israel yatoa wito kwa Marekani kutositisha Misaada nchini Misri

Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamini Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamini Netanyahu REUTERS/Baz Ratner

Israel imetoa wito kwa Marekani kutositisha Msaada wake wa mwaka wa Dola za Marekani bilioni 1.3 kwa Misri, kipindi hiki ambacho Jeshi limefanya mapinduzi dhidi ya Rais wa Misri, Mohamed Morsi.

Matangazo ya kibiashara

Chini ya Sheria ya Marekani, Misaada yote ya kijeshi na Uchumi ni lazima isitishwe dhidi ya nchi yeyote ambayo Serikali imeangushwa na Jeshi, ingawa Marekani haijaweka bayana kama kilichotokea Misri ni mapinduzi ya Kijeshi kama ambavyo Chama cha Muslim Brotherhood kinadai.
 

Kwa Mujibu wa Afisa nchini Marekani, Marekani imeombwa na Israel mara kadhaa mwishoni mwa Juma lililopita, kutositisha misaada kwa Misri kwa kuwa hatua hiyo itaathiri usalama wa Israel na kutia dosari makubaliano ya amani ya mwaka 1979 kati ya nchi hiyo na Misri.
 

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alimpigia simu Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, Waziri wa Ulinzi Moshe Yaalon akazungumza na mwenzake wa Marekani, Chuck Hagel na Mshauri wa maswala ya Usalama wa Israel , Yaakov Amidror alifanya Mazungumzo na Mwenzake wa Marekani, Susan Rice.
 

Msaada wa Marekani kwa Misri, uliokuja baada ya makubaliano ya amani, umekuwa ukielekezwa nchini Misri tangu mwaka 1979, hivi sasa Israel inahofu kuwa Sera hiyo ya Marekani ya kusitisha Misaada kwa Misri kutaondoa ari ya Misri kutiaa makubaliano hayo.
 

Eneo la Mpaka kati ya Israeli na Ukanda wa Gaza limeshuhudia hali ya Mapigano tangu kuanguka kwa utawaka wa aliyekuwa Rais wa misri, Hosni Mubarak mwaka 2011, hali ambayo ilianzisha mashambulizi nchini Israel, pia uwepo wa Majeshi ya Misri katika eneo hilo.