SYRIA

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa UN Ban Ki Moon,atoa wito kwa Syria kuacha mapigano wakati huu wa Mfungo wa Ramadhani

Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Ban Ki Moon
Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Ban Ki Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amezitaka pande zinazoendeleza mapigano nchini Syria kuacha mapigano kuupisha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Matangazo ya kibiashara

hatua hii imekuja wakati ambapo Vikosi vya Rais wa Syria Bashar Al Assad kuingia katika jimbo la Khaldiyeh mjini Homs uliokuwa ukishikiliwa na Waasi.
 

Ban ametaka Majeshi yote ya Serikali na Jeshi la wapiganaji wa Syria na kila mmoja aliyeshika Silaha kuweka silaha chini na kuacha mapigano kwa ajili ya kuuheshimu mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kuwa ni mwezi wa amani na umoja.
 

Katika kipindi hiki Ban Ki Moon ametoa wito wa kuachiwa kwa Wafungwa nchini humo.
Katika hatua nyingine Chama tawala nchini humo, Baath kimefanya mabadiliko mapya kukiwa na uongozi mpya wa Kamati kuu ya Chama hicho huku Assad akiendelea kuwa katibu mkuu wa Chama hicho.
 

Mabadiliko ndani ya Chama hicho ni ya kwanza tangu mwaka 2005 na Assad amekitaka Chama hicho kufanya kazi kwa karibu na Watu ili kumaliza mapigano nchini humo.

Chama cha Baath kimekuwa madarakani tangu tarehe 8 machi mwaka 1963.