Afghanistani

Wanamgambo wa Taliban wafunga Ofisi yao kwa muda nchini Qatar

Rais wa Afghanistani, Hamid Karzai
Rais wa Afghanistani, Hamid Karzai REUTERS/Omar Sobhani

Wanamgambo wa Taliban wamefunga Ofisi zao kwa muda nchini Qatar, ambapo kulikuwa na matumaini ya kuanza kwa mazungumzo ya amani kati ya marekani na Afghanistani, Afisa wa kundi la Wanamgambo hao amethibitisha akitoa lawama kwa kuvunjika kwa ahadi zilizotolewa.

Matangazo ya kibiashara

Ofisi hiyo ilifunguliwa tarehe 18 mwezi June ikiwa ni hatua ya kwanza katika kuelekea kwenye makubaliano ya amani baada ya miaka 12 ya mapigano,hatua ya kufungua Ofisi iliyomghadhabisha Rais wa Afghanistani Hamid Karzai.
 

Karzai alivunja Mazungumzo juu ya maswala yahusuyo Usalama kati yake na Marekani na kutishia kususia mchakato wowote wa kupatikana amani, wakati huu ambapo jitihada za kumaliza makundi ya Wanamgambo zikiendelea kabla ya Vikosi vya kigeni kuondoka mwakani.
 

Wanamgambo hao wamesema kuwa hawafurahishwi na Marekani, Serikali ya Kabul na pande nyingine zote wakidai kuwa hawajawa wakweli.
 

Marekani kwa upande wao imesema kuwa kufungwa kwa Ofisi kusiharibu mchakato wa kupatikana kwa amani.
 

Hatua hii ya Mchakato wa amani kuingiliwa na vikwazo imekuja wakati huu mbapo Taliban ilidai kuwa ilitekeleza shambulio la Bomu mjini Herakat na kusababisha watu 17 kupoteza maisha.
 

Vikwazo vya hivi dhidi ya mazungumzo ya amani, yanakuja kufuatia Gazeti moja nchini Marekani kuripoti kuwa marekani inafanya mchakato wa kuondoa Vikosi vyake haraka iwezekanavyo nchini Afghanistani kwa sababu ya kuwepo kwa hali ya Mvutano na Rais wa nchi hiyo, Hamid karzai.