Syria

UN yaridhia mwaliko wa Syria kupeleka wawakilishi kwa ajili ya mazungumzo juu ya shutma za matumizi ya Silaha za kemikali

Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Ban Ki Moon
Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Ban Ki Moon

Umoja wa Mataifa umeridhia Mwaliko wa Serikali ya Syria kuruhusu Maafisa wawili wa Umoja wa Mataifa, kwa ajili ya mazungumzo kuhusu matumizi ya Silaha za kemikali nchini humo, Msemaji wa UN ameeleza.

Matangazo ya kibiashara

Mwaliko huo wa kufanya mazungumzo umetolewa kwa Mwanasayansi Ake Sellstrom ambaye aliteuliwa na Umoja wa Mataifa kuchunguza ukweli juu ya madai ya matumizi ya Silaha za kemikali, pia Angela Kane mwakilishi kutoka Tume ya upatanishi.
 

Balozi wa Syria ndani ya Umoja wa Mataifa, Bashar Jaafari amekana kuwa Damascus inampango wa kubadilisha mwelekeo wa dhamira ya Uchunguzi wa Umoja wa Mataifa.
 

Katika hatua nyingine, Marekani imefanya uchunguzi madai ya Uruai kuwa Waasi wa Syria walitumia Gesi aina ya Sarin katika Shmabulio lao jijini Aleppo lakini imesema inaamini kuwa Upinzani hauna uwezo wa kuwa na silaha za namna hiyo.
 

Mjumbe wa Urusi ndani ya Umoja wa Mataifa alisema siku ya jumanne kuwa Wataalam kutoka nchini mwake wamekuwa katika eneo palipofanyika Shambulizi karibu na mji wa Aleppo mwezi March na kupata Ushahidi wa hilo.
 

Urusi imekuwa ikishutumiwa kuzuia juhudi za Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuruhusu Umoja wa Mataifa kuingia nchini Syria kuchunguza ukweli juu ya Shutma za matumizi ya Silaha za Kemikali.