SYRIA

Kamanda wa taifa la kiislam la Iraq atekwa na Wakurdi wa nchini Syria

Wapiganaji wa kikurdi katika mapambano dhidi ya wanajihadi
Wapiganaji wa kikurdi katika mapambano dhidi ya wanajihadi www.naharnet.com

Wapiganaji wa Kikurdi katika eneo la Kaskazini mwa Syria wamepigana vita vikali dhidi ya wanajihadi na kufanikiwa kumteka kamanda wa taifa la Kiislamu la Iraq na kundi la I-S-I-S usiku wa kuamkia leo shirika la uangalizi wa haki za binadamu nchini humo limesema. 

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo inakuja siku chache tu baada ya wapiganaji wa Kikurdi watiifu kwa chama cha Democratic Union (PYD) kuwafukuza wanajihadi wenye uhusiano kundi la Al-Nusra na Taifa la Kiislamu la Iraq na wapiganaji wa I-S-I-S kutoka mji wa Ras al-Ain.

Kabla ya kumteka nyara kamanda huyo  wapiganaji hao waliwafukuza wapiganaji wa Jihadi kutoka katika eneo la ukaguzi na kukamata silaha zao na risasi, shirika la uangalizi wa haki za binadamu nchini humo limesema.

Mikoa ya Kikurdi imekuwa ikisimamiwa na halmashauri za mitaa tangu vikoso vya Rais Bashar al-Assad vijiondoe katika maeneo hayo katikati ya mwaka 2012.