PAKISTAN-TALIBAN

Watu 10 wauawa kwenye mapigano kati ya vikosi vya Pakistan na Taliban

REUTERS/Mohammad Ismail

Watu 10 wameuawa baada ya mapigano makali kati ya Vikosi vya usalama vya Pakistani na Wanamgambo wa kiislamu kaskazini magharibi mwa nchi hiyo karibu na mpaka kati ya Pakistan na Afghanistani.

Matangazo ya kibiashara

Wanamgambo kadhaa wakiwa na silaha walivamia kituo cha ukaguzi cha mji wa Khyber ambapo wanamgambo wanane na Wanajeshi wawili waliuawa baada ya kutokea majibizano ya risasi.

Pakistani imekuwa ikipoteza kwenye mashambulizi dhidi ya makundi ya kigaidi ya Al Qaeda na Wanamgambo wa Taliban, huku Serikali ikisema kuwa zaidi ya Watu 40,000 wameuawa katika mashambulizi ya risasi na mabomu yanayotekelezwa na Wanamgambo.

Mwanzoni mwa juma hili Wanamgambo wa Taliban waliwatorosha Wafungwa takriban 250 wakiwemo Wanamgambo sugu, baada ya kufanya shambulizi katika Gereza moja kaskazini magharibi mwa Pakistan Shambulio lililogharimu maisha ya Watu 13.

Watu wapatao 12 wakiwemo askari wanne waliuawa na saba wamejeruhiwa katika shambulio hilo lililotekelezwa na wanamgambo waliokuwa wamevalia sare za polisi ambao walikabiliana vikali na vikosi vya Usalama.

Wafungwa sita kati ya waliotoroka walikamatwa baada ya msako mkali ulioendeshwa na vikosi vya usalama.