Syria

Jopo la Uchunguzi lapewa kibali kuingia nchini Syria kuchunguza Shutma za matumizi ya Silaha za kemikali

Rais wa Syria, Bashar Al Assad
Rais wa Syria, Bashar Al Assad 路透社

Umoja wa Mataifa umesema kuwa suala la kuondoka kwa jopo la Wachunguzi juu ya shutma za kutumika kwa Silaha za kemikali nchini Syria ni la uhakika Baada ya Mamlaka ya Damascus kuridhia jopo hilo kuingia nchini Syria.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa Serikali ya Syria imekubali kuingia kwa Wachunguzi hao pia imeridhia namna ambavyo Operesheni hiyo itakavyofanyika kuhakikisha kuwa inafanyika kwa usalama na namna ipasayo.

Jopo hilo litaongozwa na Mtaalamu wa maswala ya Silaha kutoka Sweeden, Ake Sellstroem litafanya uchunguzi maeneo ambayo yameelezwa kuwa Silaha za kemikali zilitumika katika kipindi cha takriban majuma mawili.
 

Operesheni hiyo ilikwama awali kutokana na hali ya kutofautiana na Rais wa Syria, Bashar Al Assad juu ya namna ambavyo uchunguzi huo utafanyika nchini humo.
 

Umoja wa Mataifa ulifikia makubaliano mwezi uliopita na Serikali ya yria juu ya Operesheni hiyo lakini ulikuwa ukisubiri ruhusa ya mwisho kutoka Damascus.
 

Moja ya maeneo yanayotarajiwa kufanyiwa uchunguzi ni pamoja na Khan al-Assal,karibu na mji wa Aleppo ambapo Serikali inasema kuwa Waasi walitumia Silaha za kemikali tarehe 19 mwezi Machi na kusababisha Takriban Watu 26 kupoteza maisha wakiwemo Wanajeshi wa Syria 16.
 

Upinzani kwa upande wao pia umenyooshea kidole vikosi vya Serikali kuwa umekuwa ukitekeleza mashambulizi kwa kutumia silaha za kemikali.
 

Ingawa Damascus imetaka Uchunguzi ulenge katika mji wa Khan al Assal pekee, Ban Ki Moon amekuwa akisisitiza kupatiwa nafasi ya kuingia katika miji mingine pia ili kufanya uchunguzi.