Wimbi la Siasa

Mgogoro wa Syria waingia katika hatua nyingine baada ya maseneta wa Marekani kuridhia mashambulizi ya kijeshi

Sauti 09:56

Mgogoro wa Syria umeingia katika hatua nyingine baada ya maseneta wa Marekani kuridhia mashambulizi ya kijeshi huku Rais wa Marekani Barack Obama akiendelea kusaka uungwaji mkono ili kutekeleza jukumu la kuishambulia kijeshi Syria. Makala ya Wimbi la Siasa juma hili inapiga kambi kuangazia hali ya mambo nchini Syria na kujibu maswali mbalimbali yanayoibuka wakati huu dunia ikiwa imegawanyika juu ya suala la Syria.