SYRIA-Diplomasia

Urusi haikubaliani na Umoja wa Mataifa kwa kuituhumu Serikali ya Bachar al Assad

RFI

Urusi imezua kupitishwa kwa azimio katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kukashifu mauji yaliyotekelezwa na majehsi ya seriklai ya Syria katika mji wa Allepo katika siku za hivi karibuni. Hii ni mara ya pili kwa Urusi kuzuia kupitsihwa azimio dhidi ya serikali ya rais Assad anayetuhumiwa kutekeleza mauji hayo tangu tarehe 15 mwezi Desemba mwaka uliopita na kusababisha mamia ya wapinzani kupoteza maisha. 

Matangazo ya kibiashara

Mashirika ya kutetea haki za Binadamu yanashtumu majehsi ya serikali kurusha makombora katika masoko, hospitali na shule na kuwaua wanawake na watoto, tuhma ambazo Damascus inakanusha.

Awali, Uingereza ilieleza kwamba Umoja wa Mataifa hauoneshi nia yoyote ya kukabiliana na mashambulizi yanayofanywa na jeshi la serikali ya Bashar dhidi ya mji wa Allepo, mashambulizi, ambayo yalisababisha watu 700 kupoteza maisha na wengine 3,000 kujeruhiwa tangu desemba 15.

Katika waraka uliyoandikwa na Uingereza, ulikemea utumiaji wa silaha na mabomu ya maangamizi viliyopigwa marufuku, katika mitaa inyokaliwa na watu wengi ya Allepo.

Uingereza iliilaumu serikali ya Syria kwamba kukiuka sheria za kimataifa.

Mkutano huo unalenga kuboresha maridhiano ili kuundwe serikali ya mpito.

Zaidi ya mataifa 30 na mashirika ya kimataifa yamealikwa kuhudhuria uzinduzi wa mkutano, ambao utafuatiwa na mazungumzo kati ya utawala na upinzani.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limegawanyika kutokana na mzozo unaoendelea nchini Syria.

Urusi na China zilisha pinga karibu mara tatu zikitumia kura yao ya turufu uingiliaji kati wa mataifa ya magharibi , ambayo yamekua yakitoa shinikizo dhidi ya rais wa Syria Bachar al-Assad.