PALESTINA-ICC

Wanaharakati wa haki za binadamu wamtolea wito Mahmoud Abbas kuitambua ICC

Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas akiombwa na mashirika yanayotetea haki za binadamu kutia sani ya kuitambua mahakama ya kimataifa ICC..
Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas akiombwa na mashirika yanayotetea haki za binadamu kutia sani ya kuitambua mahakama ya kimataifa ICC.. Reuters/Mohamad Torokman

Mashirika ya kutetea haki za bunadamu likiwemo shirika la Amnesty International juma hili yametoa wito kwa serikali ya mamlaka ya Palestina kutia saini mkataba unaotambua mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC.

Matangazo ya kibiashara

Mashirika zaidi ya kumi na saba ya ndani ya Palestina na yale ya kimataifa likiwemo shirika la Amnesty International, kwa pamoja wamemuandikia barau rais wa Mamlaka ya Palestina Mahamoud Abbas kutia saini mkataba wa Roma kujiunga na mahakama ya ICC.

Mashirika hayo kwenye maelezo yake, yamesema kuwa kujiunga kwa mamlaka ya Palestina kwa kutia saini makataba wa Roma kutaifanya nchi hiyo kupata haki hasa kwa viongozi wake ambao waliuawa ndani na nje ya palestina.

Mratibu wa shirika la Amnesty kwenye ukanda wa mashariki ya kati na Afrika Kaskazini, Philip Luther amesema kuwa mkataba huo utaiwezesha mahakama ya ICC kuwafungulia mashtaka wahalifu wa kivita waliotenda makosa ndani na nje ya mamlaka ya Palestina.

Mwezi April mwaka huu rais Abbas alitia saini mkataba wa kujiunga na mashrika 15 ya umoja wa mataifa hatua iliyopelekea kuvunjika kwa mazungumzo ya amani kati yake na Israel.

Nchi ya Israel na Marekani zimekuwa mstari wa mbele kuyashawsihi mashirika ya Umoja wa mataifa kuitambua mamlaka ya Palestina mpaka pale kutakapopatika suluhu kati yake na Israel.