UTURUKI-Ajali

Uturuki: idadi ya vifo inaendelea kuongezeka

Moja wa majeruhi katika ajali iliyotokea katika mgodi wa makaa wa Soma nchini Uturuki.
Moja wa majeruhi katika ajali iliyotokea katika mgodi wa makaa wa Soma nchini Uturuki.

Uturuki imeendelea kukabiliwa na maafa yaliyosababishwa na ajali ya moto katika mgodi wa mawe wa Soma, na kusababisha kwa sasa vifo vya watu 282 kulingana na idadi ya mwisho iliyotolewa na viongozi jana usiku.

Matangazo ya kibiashara

Hali hio inajiri wakati wito wa kuwataka wafanyakazi kuanzisha mgomo umekua ukitolewa na vyama vya wafanyakazi wa serikali.

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alikabiliwa jana na matamshi makali yaliyokua yalitolewa na waandamanaji wakimtuhumu kupuuzia suala la usalama la wachimba migodi katika sekta ya kibinafsi.

Idadi ya vifo inaendelea kuongezeka kutokana na jali ya moto iliyotokea katika mgodi wa makaa wa Soma nchini Uturuki.
Idadi ya vifo inaendelea kuongezeka kutokana na jali ya moto iliyotokea katika mgodi wa makaa wa Soma nchini Uturuki. REUTERS/ Osman Orsal

Miili mingine 90 ya watu waliyofariki katika ajali hio imepatikana katika mgodi huo wa makaa ya mawe na kufikia idadi ya watu waliyofariki 282.

Kwa mujibu wa viongozi wa Uturuki, idadi hio haijawa rasmi kwani kuna wachimba migodi wengine ambao bado wamefukiwa na udongo, baada ya ajali hio iliyosababishwa na moto kutokea.

“Hadi jana usiku kwenye saa mbili kamili, tulikua na idadi ya watu 282 waliyofariki”, waziri wa nishati Taner Yildiz, ameambia vyombo vya habari.

Ni tukio baya kuwahi kutokea na ni pigo kubwa kwa Uturuki, ambapo idadi hio huenda ikaongezeka kwani hakuna matumaini ya kuwapata tena watu waliyo hai ambao bado wamefukiwa na udongo.

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, amesema uchunguzi imeanzishwa ili kujua chanzo cha ajali hio.

Swala na sherehe za mazishi zitaandaliwa leo mchana, amesema waziriYildiz.

Wazazi wa wahanga katika ajali ya moto iliyotokea katika mgodi wa makaa wa Soma nchini Uturuki.
Wazazi wa wahanga katika ajali ya moto iliyotokea katika mgodi wa makaa wa Soma nchini Uturuki.

Familia za wahanga zimekua zikiondoa miili ya ndugu zao katika chumba cha kuhifadhi maiti kiliyotengwa katika eneo la Kirkagaç, kijiji kilioko kwenye kilomita kadhaa na mji wa Soma. 

Wakishindikizwa na polisi, wazazi wa wahanga wamesumbuka kutambua miili ya ndugu zao kutokana na jinsi ilivyokua imeharibika.