Syria-msamaha

Rais wa Syria Bashar Al Assad atangaza msamaha wa jumla

Bashar al Assad akizungumza na kituo cha habari 20/01/2014
Bashar al Assad akizungumza na kituo cha habari 20/01/2014 REUTERS

Rais wa Syria Bachar Al Assad ametangaza msamaha wa jumla kwa makosa yote yaliotekeleza hadi leo jumatatu, uamuzi ambao unachukuliwa ikiwa ni juma moja baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo. Duru za wizara ya sheria zimearifu kuwa hatuwa hiyo imechukuliwa ili kudumisha maridhiano na uwinao baada ya jeshi la nchi hyo kupata ushindi mkubwa dhidi ya waasi.

Matangazo ya kibiashara

Hii ni mara ya tano rais Assad kutangaza msamaha wa jumla tangu kuanza kwa maandamano March 2011, yaliogeuka na kuwa machafuko ya umwagaji wa damu kati ya jeshi la serikali na waasi.

Wananchi wa Syria wakipiga kura kwenye Ubalozi wa Jordan
Wananchi wa Syria wakipiga kura kwenye Ubalozi wa Jordan REUTERS

Rais Assad ambaye serikali yake inaonakuwa hakuna uasi nchini mwake bali kuna ugaidi, ilitangaza msamaha wa jumla Mei 31, Juni 21 na Januari 15 mwaka 2012 pamoja na April 16 mwaka 2013.

Msahama huu wa leo Jumatatu unakuja baada ya kuchaguliwa tena kwa rais Assad katika uchaguzi mkuu wa rais wa Juni 3 ambao ulipingwa vikali na upinzani pamoja na washirika wake.

Hayo yanajiri wakati huu wapiganaji 45 wa kundi la kiislam wakipoteza maisha katika mapigano na kundi lingine lenye mafungamano na Alqaeda, duru za shirika linalo tetea haki za binadamu zimearifu

Makundi hayo yaliungana ili kupambana na serikali ya rais Assad kabla ya kuwa mahasimu baada ya kundi la wanamgambo ambao wanapigana pia nchini Iran kulishambulia kundi la Al Nosra lenye mafungamano na Alqeda kwa tuhuma za kuendesha mauaji ya kikatili.

Katika hatuwa nyingine waziri mkuu nchini Qatar Cheikh Abdallah Ben Nasser Ben Khalifa Al Thani ameendelea kulitolea shinikizo baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuingilia kati na kulazimisha utishwaji wa mapigano nchini Syria na kuhakikisha wananchi wa Syria wanamaliza tofauti zao.