SYRIA-Siasa

Syria : Bashar Al Assad atawadhwa kuwa rais

Rais wa Syria, Bashar Al Assad, akitawadhwa kuwa rais kwa muhula wa tatu.
Rais wa Syria, Bashar Al Assad, akitawadhwa kuwa rais kwa muhula wa tatu. Reuters/Sana/Handout

Rais wa Syria Bashar Al Assad ametawadhwa kuwa rais kwa muhula watatu, wakati wa sherehe ambazo zimefanyika kwenye ukumbi wa ikulu mjini Damas. Bachar Al Assad amekula kiapo mbele ya wabunge na viongozi mbalimbali walioalikwa kuhudhuria sherehe hizo.

Matangazo ya kibiashara

Mpiganaji wa kundi la waasi wa Syria,.
Mpiganaji wa kundi la waasi wa Syria,. REUTERS/Goran Tomasevic

Syria inakabiliwa na mapigano kati ya jeshi la serikali na waasi yanayodumu kwa sasa miaka mitatu, na ambayo yamesababisha vifo vya watu 170.000.

Wakati huo huo watu wanne wameuawa jumatano wiki hii katika mashambulizi ya mabomu yaliyorushwa na waasi katika mji mkuu wa taifa hilo, Damas, shirika la habari la serikali Sana limefahamisha.

Syria inaendelea kukabiliwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
Syria inaendelea kukabiliwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. REUTERS/Bassam Khabieh

“Watu wanne wameuawa na wengine 22 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya mabomu yaliyorushwa na waasi katrika mtaa wa Chaalane katikati mwa mji wa Damas”, Sana imeeleza, ikitaja kuwa taarifa hizi ni kwa mujibu wa vyanzo vya polisi.

Wakaazi wa Damas wamesikia mabomu yakilipuka, huku idadi ya watu waliouawa na kujeruhiwa na mabomu hayo wakibebwa kwenye vitua vya afya viliyo karibu.
Waasi wamesema kwamba mtu mmoja ndiye ameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulio hilo.

Mabomu yanayorushwa na waasi huwa yakidondoka katika mji wa Damas wakati jeshi la serikali likiendelea na mashambulizi yake ya anga katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi pembezuni mwa mji mkuu, Damas.

Mashambulizi hayo yametokea dakika chache baada ya hotuba ya rais Bashar Al Assad aliyoitoa katika ikulu magharibi mwa mji wa Damas.

Rais Assad iko mamlakani tangu mwaka 2000, amekula kiapo, huku akishikilia Qor'an kwenye mkono wake wa kulia.