IRAN-ISRAELI-PALESTINA-Usalama

Iran : Ali khamenei atolea wito ulimwengu wa kislamu kuwapa silaha wapalestina

Ayatollah Ali Khamenei, kiongozi wa kidini nchini Iran.
Ayatollah Ali Khamenei, kiongozi wa kidini nchini Iran. Reuters

Iran ambayo haitambui kuwepo kwa taifa la Israeli, imelani mashambulizi ya anga ya jeshi la Israeli katika Ukanda wa Gaza. Iran ambayo imekua mtetezi wa makundi ya kislamu imesema haikubaliani na kile Israeli inachofanya kwa sasa katika ukanda wa Gaza.

Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake ya kuadhimisha kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan, ambayo imeonekana ni ya kusisimua, kiongozi wa kidini Ayatollah Ali Khamenei, amelani mashambulizi ya Israeli dhidi ya Gaza, ambayo yamesababisha watu 1.100 kuawa kwa kipindi cha wiki tatu, huku akitaja Israeli imetekeleza mauaji ya kimbari.

Mbele ya mamia kwa maelfu ya waumini waliokusanyika kwa ibada ya swala ya kumalizika kwa mwezi mtukufu wa ramadhan, Khamenei ametoa kauli kali dhidi ya Israeli, na kuifananisha na “mbwa mwenye kichaa”, ambayo inatekeleza “mauaji ya halaiki “dhidi ya raia wa Gaza. Hata hivo Khamenei amepinga kauli ya rais wa Marekani, Barack Obama ya kutaka makundi ya kislamu nchini Palestina yapokonywe silaha.

“Rais wa Marekani ameanzisha hivi karibuni zowezi baada ya kuongea kwamba makudi ya kislamu nchini Palestina yapokonywe silaha kwa lengo la kudhohofisha itikadi ili asijibu tuhuma za uhalifu zinazomkabili. Sisi tutapinga kauli hiyo na kubaini kwamba dunia nzima hususan ulimwengu wa kislamu tunapaswa kuwasaidia raia wapalestina kwa kuwapa silaha”, amesema Khamenei.

Viongozi wa Irani wamethibitisha mara kadhaa kwamba wamekua wakiwapa wapiganaji wa kipalestina mafuzo ya kiteknolojia ya kutengeneza makombora wanayotumia kwa kurusha katika miji ya Israeli. Iran ilisaidia pia kundi la Hezbollah nchini Libanon kutengeneza makombora ambayo yana uwezo wa kwenda hadi maeneo yote ya nchi ya Israel.