ISRAELI-HAMAS-UN-MAREKANI-Kusitisha mapigano-Usalama

Jonh Kerry atangaza makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda wa saa 72 Gaza

John Kerry, en déplacement en Inde, a annoncé un cessez-le-feu de 72 heures dans la bande de Gaza
John Kerry, en déplacement en Inde, a annoncé un cessez-le-feu de 72 heures dans la bande de Gaza REUTERS/Lucas Jackson

Wakati alipokua ziarani katika mji mkuu wa India, New Delhi, John Kerry ametangza kwamba Hamas na Israeli wamekubaliana kusitisha mapigano katika ukanda wa Gaza kwa muda wa saa 72 kuanzia saa 11 asubuhi saa za kimataifa ijumaa wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani, amesema tangazo hilo la kuitaka Israeli na Hamas kusitisha mapigano limetolewa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon kwa ushirikiano na Marekani. Mazungumzo kati ya Israeli na Palesrtina yanatazamiwa kuanza ijumaa wiki hii katika mji mkuu wa Misi Cairo, amesema afisa mmoja wa Marekani. Ujume wa Palestina utateuliwa na rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas, lakini yeye hatahudhuria katika mazungumzo hayo.

Hamas kupitia msemaji wake, Sami Abou Zouhri, imekubali kusitisha mapigano. “ Tumekubali kusitisha mapigano kwa muda wa saa72 kuanzia saa 2 asubuhi leo ijumaa kwa kuitikia wito uliyotolewa na Umoja wa Mataifa na vilevile kutokana na hali inayowakabili raia wtu, ili kuruhusu misaada iweze kuwafikia”, amesema Abou Zouhri. Lakini Hamas itatekeleza makubaliano hayo iwapo,upande mwengine utayaheshimu, ameongeza Abou Zouhri.

Hata Israeli imekubali kusitisha mapigano, hata kama kulingana na chanzo kiliyokaribu na waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, kimeliambia shirika la habari la Ufaransa kwamba makubaliano hayo yatatekelezwa kwa ridhaa ya baraza la kitaifa la usalama na waziri wa ulinzi.

 ■ « Operesheni ya kujihami » ya Israeli inaendelea

John Kerry ameongeza kwamba jeshi la aridhini la Israeli litaendelea kushikilia na kuimarisha usalama kwenye ngome zao, na litaendelea na “operesheni zake za kujihami” kwa muda wote wa kusitishwa kwa mapigano.

Kufuatia kusitishwa kwa mapigano hayo kwa muda wa saa72, raia wa Gaza watapata nafasi kupata misaada ya chakula na maji, kuzika ndugu zao na kushughulikia majeruhi.

 ■ Mapigano ya mwisho

Wapalestina wanane wameuawa kwa makombora yaliyofyatuliwa na vifaru vya Israeli, katika mji wa Khan Younès, kusini mwa ukanda wa Gaza, msemaji wa idara ya huduma za dharura katika ukanda wa gaza ,Achraf al-Qodra, amesema. Mwanamke mmoja na watoto wawili ni miongoni mwa watu waliouawa. Saa moja baadae watu sita waliuawa katika mashambulizi ya anga katika mji huo wa Khan Younès. Takribani wanajeshi watano wa Israeli wameuawa alhamisi wiki hii kwenye mpaka wa Israeli na Gaza, duru za kijeshi zimearifu.